IQNA

Rais Rouhani wa Iran

Ushirikiano uendelee hadi ugaidi uangamizwe kikamilifu

18:12 - December 05, 2017
Habari ID: 3471296
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa leo, nguzo kuu za ugaidi katika eneo la Asia Magharibi zimeporomoka na kuongeza kuwa, 'sehemu kubwa ya njama za madola makubwa duniani, uistikabri na Uzayuni dhidi ya mataifa ya eneo zimegonga mwamba.'

Hassan Rouhani, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo katika Kongamano la 31 la Kimataifa la Umoja wa Kiislamu mjini Tehran ambapo awali ametoa salamu za kheri na fanaka kwa munasaba wa Maulidi ya Mtume wa Uislamu Muhammad Al Mustafa SAW, na Imam Jaafar Sadiq AS, Imamu wa Sita wa Mashia, na Wiki ya Umoja wa Kiislamu. Rais Rouhani amesema wadau wote katika eneo wataendelea kushirikiana katika vita dhidi ya ugaidi hadi utakapoangamizwa kikamilifu.

Rais wa Iran ameashiria ushujaa wa wanamapambano ambao wamekuwa wakikabiliana na magaidi katika eneo na kusema walichokifanya ni kwa maslahi ya mataifa ya eneo. Ameongezwa kwamba inasikitishwa kuona kuwa wakati wote wanaotaka amani na usalama duniani wanashukuru wanamapambano na wanamuqawama waliokabiliana na magaidi, baadhi wanapanga njama za kudhoofisha kambi hiyo iliyokabiliana na ugaidi.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria namna baadhi ya nchi za eneo zinavyotangaza  urafiki wa wazi na utawala wa Kizayuni pamoja na maadui wa kambi ya muqawama na kusema: "Wanazuoni, wasomi na vijana hawataruhusu kufanikiwa njama hii chafu ya maadui dhidi ya muqawama."

Rais wa Iran ameendelea kusema kuwa, Marekani, Waistikbari wa kimataifa na Wazayuni wamehusika katika mauaji ya vijana wa eneo la Asia Magharibi na hivyo wanapaswa kuwajibika mbele ya mataifa ya dunia. Aidha amesema mbali na mauaji, Wazayuni na Wamarekani pia wameharibu turathi za ustaarabu wa eneo na kuzibadilisha kuwa magofu. Rais wa Iran pia amehoji ni kwa nini Wazayuni na Wamarekani wanatuma silaha na mabomu kwa lengo la kuwaangamiza watu wa Yemen huku pia akiashiria njama zinazoendelea za maadui dhidi ya eneo la Afrika Kaskazini.

Rais Rouhani amesema umoja ndio njia pekee ya kuelekea katika mkondo wa ustaarabu mpya wa Kiislamu. Amesisitiza kuhusu kusimama kidete kwa ajili ya ukombozi wa Palestina kama yalivyosimama kidete mataifa ya Kiislamu kukabiliana na mabebeuur na kupata uhuru. Amesema katika kukabiliana na Wazayuni maghaisbu na ugaidi kuna haja ya kuwepo umoja ili kupata ushindi.

Mkutano wa 31 wa Kimataifa ya Umoja wa Kiislamu umeanza leo hapa Tehran kwa kuhuhudriwa na wageni zaidi ya 500 wa kutoka Iran na nchi za kigeni chini ya nara ya , "Umoja na Mahitajio ya Ustaarabu Mpya wa Kiislamu." Mkutano huo utaendelea hadi tarehe saba Disemba.

3464613

captcha