IQNA

Wanafunzi 14,000 wajisajili kwa ajili ya mashindano ya Qur'ani Qatar

11:37 - December 11, 2017
Habari ID: 3471304
TEHRAN (IQNA)-Wanafunzi wapatao 14,000 hadi sasa wamejisajili kushiriki katika awamu ya 57 ya Mashindano ya Qurani katika shule za Qatar.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wanafunzi waliojisajidi ni kutoka shule za umma na pia shule binafsi katika nchi hiyo ndogo ya Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi.

Mashindano hayo yameandaliwa Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kiislamu Qatar kwa ushirikiano na wizara ya elimu nchini humo. Usajili wa washiriki wa mashindano hayo ulianza kati kati ya mwezi Oktoba na utaendelea hadi Februari 11.

Wanaoandaa mashindano hayo wametoa wito kwa wanafunzi waendelee kujisajili kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yatafanyika baadaye mjini Februari mwakani.

3464654

captcha