IQNA

Ustadh Sagar wa Kenya Ashika Nafasi ya Pili Mashindano ya Qur'ani Misri

1:08 - March 31, 2018
Habari ID: 3471449
TEHRAN (IQNA)-Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Misri wametangazwa ambapo ambapo Ustadh Haitham Sagar kutoka Kenya ameibuka wa pili katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani kwa wale ambao Kiarabu si lugha yao ya asili.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani kikamilifu kwa wale ambao lugha yao asili si Kiarabu nafasi ya kwanza imechukuliwa na Mohammad Mujahidul Islam wa Bangladesh na nafasi ya pili ameshika Ustadh Haitham Sagar Ahmad wa mji wa Mombasa nchini Kenya huku nafasi ya tatu ikuchukuliwa na Mohammadev Mohammadi wa Tajikistan.

Katika kitengo chakuhifadhi Qur'ani kikamilifu amabcho kilijumuisha wale ambao lugha yao asili ni Kiarabu na wale ambao lugha yao asili si Kiarabu nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Ismail Fuad Ismail wa Misri nafasi ya pili pia maechukua Mmisri Mohammad Said Dhaifullah huku Umar Yusuf wa Kuwait akiibuka wa tatu.

Mashindano ya 25 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Misri yalianza Machi 24 mjini Cairo ambapo yanalidhuriwa na wawakilishi wa nchi 50 na kumalizika Alhamisi  tarehe 29.

Katika sherehe za ufunguzi zilihudhuriwa na Sheikh Mohamma Mokhtar Gomaa, Waziri wa Wakfu wa Misri na wageni wengine waalikwa. Akihutubu katika kikao hicho Sheikh Abdul Fatah Al Qussi, mwanachama wa Baraza la Maulamaa wa Misri katika hotuba ya ufunguzi amesema lendo la kuandaa mashindano hayo, ni kuwasilisha taswira sahihi ya Qur'ani na Uislamu kinyume na magaidi wanayotaka kuuchafulia Uislamu na Qur'ani jina.

/3702372

 

captcha