Kwa mujibu wa taarifa, al-Sudais ambaye ni mfanyakazi wa utawala wa Saudia, aliulizwa maswali magumu na mmoja wa waumini waliofika kusikiliza hotuba yake katika msikiti mmoja mjini Geneva lakini hakuwa tayari kujibu maswali hayo. Mwislamu aliyekuwa na hasira anasikika katika video hiyo akimuuliza al-Sudais hivi: “Ni vipi unahubiri kuhusu amani wakati munawawekea mzingiro na kuwanyima chakula ndugu zenu Yemen na Qatar?”
Al Sudais anaonekana akitoka katika msikiti pasina kujibu maswali ya mwenye kuuliza. Mwislamu huyo aliyepata ujasiri wa kumuuliza al-Sudais ni raia wa Algeria na alimtaka pia ajibu kuhusu kuhusika Saudia katika mapindizu ya serikali za Algeria mwaka 1992 na pia mapinduzi ya miaka ya hivi karibuni huko Misri na Uturuki. Aidha Mualgeria huyo aliituhumu Saudia kuwa inashirikiana na Marekani katika kuvuruga amani huku akimtaja al-Sudais kuwa mhubiri wa urongo ambaye anatoa fatua za kuhalalisha mauaji ya Waislamu nchini Yemen. Wakati baadhi ya hadhirina msikitini walipojaribu kumyanamzisha wakidai kuwa kauli yake inaibua fitinah, alijibu kwa kusema kunyamaza kimya ni fitina huku akiitaja Saudia kuwa mtumwa wa Marekani.