IQNA

Imamu aendesha baiskeli kutoka Macedonia hadi Makka kwa ajili ya Hija

12:35 - July 11, 2018
Habari ID: 3471590
TEHRAN (IQNA)- Wanaume wawili Waislamu kutoka mji wa Tetova nchini Albania hivi sasa wako safarini kuelekea katika mji mtakatifu wa Makka kutekeleza ibada ya Hija kwa baiskeli.

Imamu wa msikiti, Sheikh Amir Aslani akiwa na rafiki yake ambaye ni mwendeshaji baiskeli mtaalamu, Senad Idrisi, wameamua kutumia baiskeli wakifahamu usafiri huo utakuwa na changamoto nyingi. Lakini wamesema wanataka kuhisi matatizo ambayo Waislamu wa karne za nyuma walikumbana nayo wakati walipokuwa wakitumia miezi kadhaa kusafiri kutekeleza ibada ya Hija ambayo ni kati ya nguzo za Uislamu.

Safari hayo hiyo inatazamiwa kuchukua muda wa wiki sita na wawili hao watapitia nchi tano kabla ya kufika Makka. Tayari wameshaondoka Macedonia na kuiniga katika nchi jirani ya Albania na wako njiani kuelekea Ugiriki. Baada ya hapo watavuka Bahari ya Aegean na kuingia Uturuki na kisha kuvuka Bahari ya Mediterranea hadi Misri na kuelekea Ghuba ya Aqaba na kupanda meli itakyoawavukisha hadi Hijaz (Saudia) na kisha watatumia baiskeli kuelekea hadi miji mitakatifu ya Makka na Madina.

"Tayari tumekumana na mvua kali Albania.  Tunafahamu kuwa tutaendesha baiskeli katika msimu wa joto katika njia iliyosalia na tuko tayari kwa changamoto zozote zile," amesema Sheikh Aslani.

Anaongeza kuwa, mbali na kutekeleza ibada ya Hija pia wanalenga kutembelea maeneo ya kihistoria nchini Uturiki na Misri. Aidha anasema safari yao kwa baiskeli pia inalenga kuwahimiza Waislamu wenye uwezo sasa na vizazi vijavyo kutekeleza ibada ya Hija hata kama kutakuwa na ugumu njiani.

Jamhuri ya Macedonia ni nchi iliyo katika Rasi ya Balkan kusini mashariki mwa bara Ulaya. Macedonia ilikuwa sehemu ya Yugoslavia ya zamani na ilijitangazia uhuru mwaka 1991. Waislamu wanakadiriwa kuwa karibu asilimia 35 ya watu wote milioni mbili nchini Macedonia na inatabiriwa kuwa Uislamu utazidi kuenea kwa kasi katika nchi hiyo ya Ulaya na hata baadhi ya tafiti zinasema idadi ya Waislamu itapindukia ile ya Wakristo nchini humo ifikapo mwaka 2050. 

3466252

captcha