Inafaa kuashiria kuwa, Saudia ilianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni mwa mwezi Machi 2015 kwa lengo la kuipundua serikali ya nchi hiyo. Vita hivyo vimesababisha maafa makubwa ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na kuwaua raia wasiopungua 15,000 wasio na hatia. Idadi kubwa ya watoto na wanawake ni miongoni mwa walipoteza maisha huku miundo msingi ya nchi hiyo kama vile shule, mahospitali, madaraja n.k ikiharibiwa kabisa.