IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Watawala wa Marekani ni wapumbavu wa daraja la kwanza

11:52 - January 10, 2019
Habari ID: 3471802
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria kuendelea kudhoofika mpaka leo vyombo vya mikakati na mahesabu vya Marekani ni ukweli halisi wa mambo na akafafanua kwa kusema: "Baadhi ya viongozi wa Marekani hujifanya na hutaka waonekane wendawazimu, tab'an mimi hili sikubaliani nalo, lakini lililo hakika, wao ni "wapumbavu wa daraja la kwanza".

Ayatullah Sayyed Ali Khamenei, ameyasema hayo Jumatano asubuhi mjini Tehran mbele ya hadhara ya maelfu ya wananchi wa mji wa Qom, kwa mnasaba wa kuadhimisha mwamko wa kihistoria ya wananchi hao, ya tarehe 9 Januari 1978 (19 Dei 1356).

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa: Suala la asili na la msingi la makabiliano ya Marekani na taifa la Iran, ni makabiliano ya kihistoria na ya dhati baina ya haki na batili, kwa sababu Uistikbari na Ukoloni unanawiri kwa kunyonya damu za mataifa; na Mapinduzi ya Kiislamu yamesimama kidete kukabiliana na dhulma hiyo ya wazi kabisa na kufanya juhudi pia za kuyaamsha mataifa.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, kusikika mayowe ya "Mauti kwa Marekani" katika nchi kadha wa kadha ni jambo ambalo halijawahi kutokea na ni ishara ya mafanikio iliyopata Iran; na akabainisha kwamba: Uistikbari unatumia kila njia kuyapotosha mataifa kupitia "Uenezaji Chuki Dhidi ya Iran", "Uenezaji Chuki Dhidi ya Uislamu" na "Uenezaji Chuki Dhidi ya Ushia", lakini binafsi yao, mataifa hayana uadui wowote na Iran ya Kiislamu, na kila yanapodhihirikiwa na ukweli huwa yanaiunga mkono.

Ayatullah Khamenei aidha ameusia kutokuwa na fikra na mitazamo ya kijuujuu kuhusu chanzo na sababu hasa ya uadui wa madhalimu wa dunia dhidi ya Iran, na akafafanua kwa kusema: Sababu kuu ya uadui huu ni "dhati na hakika ya harakati adhimu ya Mapinduzi ya Kiislamu, ushujaa, kujitolea mhanga na uaminifu wa wananchi, pamoja na Mfumo kushikamana kikamilifu na kwa kudumu na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu", ambapo kama, kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu, harakati hii itayafikia malengo iliyoyakusudia, itaufungisha virago Uistikbari na Ukoloni wa Magharibi.

Ayatullah Khamenei aidha amesema ni kichekesho kwa baadhi ya watawala wa madola ya Magharibi kuiutaka Iran ijunuze haki za binadamu kutoka kwa utawala wa Saudia.

3779781

captcha