IQNA

Msikiti wa Sāheb ul Amr, Kituo katika Historia

Msikiti wa Sāheb ol Amr ni kati ya misikiti mikongwa na kale zaidi katika mji wa Tabriz nchini Iran. Jengo hili lilijengwa mwaka 1636 Miladia na Shah Tahmasp wa Kwanza katika zama za silsila ya watawala wa Safavi na mwanzoni ulikuwa unamilikiwa na mfalme. Baada ya hujuma ya jeshi la Othmaniya Iran, msikiti huo uliharibiwa kikamilifu. Msikiti huu ulijengwa upya na na unapatikana katika Barabara ya Daraiee mjini Tabriz.