IQNA

Afrika Kusini iko mbioni kufunga ubalozi wake Israel

17:38 - October 15, 2019
Habari ID: 3472173
TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Afrika Kusini imetangaza kuwa inaendeleza mchakato wa kufunga ubalozi wake katika utawala wa Israel mwaka mmoja baada ya kumuondoa balozi wake Tel Aviv.

Hayo yamebainika katika jibu ambalo Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametumba bunge kujibu swali la mbunge Munzoor Shaik-Emam kutoka chama cha National Freedom, aliyetaka kujua uamuzi wa kufunga ubalozi huo umefika wapi.

Mwaka 2017, Chama tawala cha Kongresi ya Taifa cha Afrika Kusini (ANC) kilitangaza katika mkutano wake wa kitaifa kuhusu kushusha hadhi ya uhusiano wa nchi hiyo na utawala wa Kizayuni wa Israel. Mkutano wa taifa wa chama tawala ANC, ambao unatambulika kama kikao cha ngazi ya juu cha kutoa maamuzi ya chama kwa sauti moja uliamua kuchukuliwa haraka na bila ya masharti yoyote hatua ya kushusha hadhi ya ubalozi wa Afrika Kusini huko Israel na kuwa ofisi tu ya uratibu. Hatua hiyo ilichukuliwa kufuatia kikithirji jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina hasa katika Ukanda wa Ghaza.

Ramaphosa amesema hadhi ya ubalozi wa Afrika Kusini mjini Tel Aviv itashushwa na kuwa ofisi ya mawasiliano tu.

Chama tawala cha African National Congress (ANC) nchini Afrika Kusini tayari kimepitisha kwa kauli moja na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wananchi wa Palestina za kukomboa nchi yao inayokaliwa kwa mabavu na Israel.

3850166

captcha