IQNA

Johnson: Uingereza haiafiki utawala wa Kizayuni kuteka Ukingo wa Magharibi

22:27 - July 01, 2020
Habari ID: 3472919
TEHRAN (IQNA) - Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema nchi yake inapinga hatu aya utawala wa Kizayuni wa Israel kuteka eneo zaidi la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Katika makala aliyoandika katika gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth, Johnson ametahadharisha kuwa pendekezo la kupora zaidi eneo la Ukingo wa Magharibi ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa. Amesema amesikitishwa na pendekezo hilo la Israel la kupora ardhi zaidi za Wapalestina.

Waziri Mkuu wa Utawala haramu wa Israel Benjamin Netanyahu, ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Likud na Benny Gantz kiongozi wa chama cha Blu na Nyeupe, walifikia makubaliano ya kutwaa asilimia 30 ya eneo la Palestina la Ukingo wa Magharibi na kuliunganisha na ardhi nyingine zilizoghusubiwa za Palestina ifikapo mwezi Julai mwaka huu wa 2020, hatua ambayo imeendelea kukabiliwa na malalamiko ya kila upande.  Uamuzi huo unatathminiwa kuwa ni sehemu ya mpango wa kibaguzi wa Marekani wa Muamala wa Karne.

Makundi ya Palestina na wanaharakati mbalimbali hata wa barabni Ulaya wameendelea kupinga vikali mpango huo wa Israel.

Kutokana na mashinikizo ya jamii ya kimataifa na maonyo yalitolewa na makundi ya muqawama katika eneo la Asia Magharibi, utawala wa Kizayuni wa Israel umeakhirisha mpango huo wa kuanza kutwaa maeneo ya Ukingo wa Magharibi na kuyaunganisha na ardhi za Palestina zilizoghusubiwa kuanzia Julai mosi. Utawala huo ghasibu kupitia Wizara ya Vita umedai kuwa eti umeakhirisha mpango huo kutokana na janga la corona. 

Jumatatu, Michelle Bachelet, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa alisema kuwa, mpango wa Israel wa kupora ardhi zaidi za Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuziunganisha na ardhi nyingine za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu ni kinyume cha sheria na kuitaka Tel Aviv iachane na mpango huo.

3908141/

captcha