IQNA

Msomi wa Malaysia

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanaweza kuwa kigezo kwa ummah wa Kiislamu + Video

19:57 - February 03, 2021
Habari ID: 3473617
TEHRAN (IQNA)- Msomi wa Kiislamu nchini Malaysia amesema Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yanaweza kuwa kigezo kwa ummah wa Kiislamu duniani katika mapambano dhidi ya udikiteta na ukosefu wa uadilifu.

Akizungumza katika warsha iliyofanyika kwa njia ya intaneti kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 42 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Sheikh Muhammad Azmi Abdulhamid, mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano la Asasi za Kiislamu Malaysia amesema Mapinduzi ya Kiislamu yaliweza kuleta mwamko na ilhamu katika ummah wa Kiislamu na dunia nzima kwa ujumla kutokana na muelekeo wake wa kukabiliana na ubebebru wa madola ya Magharibi na harakati zilizo dhidi ya Uislamu duniani.

Sheikh Abdulhamid amekumbusha kuwa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalifanikiwa kutokana na sababu kadhaa na moja ya sababu hizo ni kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kiuchumi na dhulma. Aidha amesema Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalikuwa ni kwa ajili ya heshima ya Uislamu ambao ni msingi wa utamaduni na itikadi za watu wa Iran.

 

3950178

captcha