IQNA

Msomi wa Kiislamu kutoka Ghana awapa motisha Waislamu kukubali chanjo ya Corona Uingereza

14:04 - April 29, 2021
Habari ID: 3473861
TEHRAN (IQNA)- Msomi na mhubiri wa Kiislamu kutoka Ghana amefanikiwa kuwashajiisha Waislamu wengi nchini Uingereza na kwingineko kukubali chanjo ya COVID-19 au corona.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sheikh Nuru Mohammed, Imamu wa Msikiti wa Al Abbas mjini Birmingham Uingereza amekuwa na nafasi muhimu katika kuwahimiza Waislamu wengi waafiki kudungwa chanjo ya corona.

Sheikh Nuru, ambaye amehitimu katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW cha mjini Qum nchini Iran, anasema wakati wa kuanza zoezi la chanjo ya corona alitambua kuwa waumini wengi katika msikiti aliokuwa akiswalisha walikuwa na shaka kuhusu chanjo.

Anasema alijitahidi kufafanua kuhusu umuhimu wa chanjo ya corona katika hotuba zake za Ijumaa ambazo alikuwa akizituoa kwa njia ya intaneti.  Aidha wasimamizi wa msikiti wa Al Abbas waliafiki utumike kama kituo cha chanjo, na hivyo ukawa msikiti wa kwanza Uingereza kufanya hivyo.

Sheikh Nuru binafsi pia alichanjwa na hivyo akawa mfano kwa waumini na hatua yake hiyo ilikuwa na mafanikio. Anasema baada ya chanjo yake, waumini katika msikiti walimjulia hali na baada ya kubaini chanjo haikuwa na madhara waliafiki kuchanjwa. Hivi sasa mamia ya waumini katika msikiti huo wamechanjwa na pia karibu watu 15,000 wa mtaa wa karibu na msikiti wamechanjwa katika kituo cha chanjo hapo msikitini.

Sheikh Nuru anasema hicho kitendo cha wasiokuwa Waislamu kuchanjwa hapo msikitini pia kimewapa fursa wengi kuujua msikiti na kuufahamu Uislamu.

Baada ya Msikiti wa Al Abbas kuafiki kuwa kituo cha chanjo hivi sasa misikiti mingine 50 kote Uingereza inatumika kama vituo vya chanjo.

Dkt. Parth Patel wa Chuo Kikuu cha London anasema viongozi kama Sheikh Nuru wamekuwa na nafasi muhimu katika kuelimisha jamii kuhusu chanjo.

Kuna sababu za kihistoria ambazo zimepelekea watu wenye asili ya kusini mwa Asia na Afrika kushuku chanjo ya corona ikiliganishwa na wazungu nchini humo. Jamii hizo mbili kwa muda mrefu zimekuwa zikibaguliwa na hivyo ni rahisi kutilia shaka chochote kinachopendekezwa na serikali.

Murtaza Master, mtaalamu wa dawa ambaye huswali katika Msikiti wa Al Abbas anasema kwa kuzingatia kuwa watu wa jamii za waliowachache wamekuwa wakitumia kufanyia dawa majaribio wengi wameshuku chanjo ya corona iliyopendekezwa na serikali. Ametoa mfano wa wanasayansi wawili wa Ufaransa ambao walitaka Waafrika wafanyiwe majaribio chanjo ya corona kabla ya maeneo mengine duniani.

روحانی شیعه بیرمنگام؛ سوژه شبکه آمریکایی

Mmoja kati ya wanazuoni wa Ahul Sunna akichanjwa katika Msikiti wa Al Abbas mjini Birmingham 

3967910

captcha