IQNA

Ni kwa nini utawala wa Kizayuni wa Israel umekithirisha jinai katika mji wa Quds?

15:01 - May 09, 2021
Habari ID: 3473891
TEHRAN (IQNA)- Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambayo pia ilikuwa Siku ya Kimataifa ya Quds ilishuhudia hujuma mpya askari wa utawala haramu wa Israel dhidi ya Msikiti Mtakatifu wa Al Aqsa mjini Quds (Jerusalem).

Askari hao wa utawala dhalimu wa Israel waliwashambulia kinyamai Wapalestina waliokuwa wanatekeleza ibada zao katika msikiti huo ambao ni qibla cha kwanza cha Waislamu.

Shirika la Hilali Nyekundu ya Palestina limesema Wapalestina wasiopungua 205 wamejeruhiwa katika hujuma hiyo.

Kabla ya hapo pia askari hao waliwashambulia Wapalestina katika eneo la Bab al-Amoud na kujeruhi mamia kati yao. Swali hapa ni kwamba, je, nini chanzo cha mashambulio ya mara kwa mara yanayofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia?

Sababu kuu ya hujuma ya askari wa Israekl dhidi ya raia wa Palestina ni mashambulio yanayotekelezwa kila siku na askari hao ghasibu kwenye maoneo ya Wapalestina na kuwabomolea nyumba zao kwa lengo la kuwafukuza kwenye maeneo hayo.

Mtaa wa Sheikh Jarrah

Hivi karibuni askari hao walivamia na kubomoa kiholela makazi ya Wapalestina katika mtaa wa Sheikh Jarrah katika mji mtakatifu wa Quds. Eneo hilo ambalo lilitekwa na kukaliwa kwa mabavu na Wazayuni mwaka 1967 lina zaidi ya Wapalestina 3000 na linachukuliwa kuwa mstari wa mbele wa kutetea Msikiti wa al-Aqsa. Kwa maneno mengine ni kwamba mtaa huo uko kwenye kitovu cha mji wa Quds na unayaunganisha maeneo ya mashariki na magharibi mwa mji huo.

Ni kutokana na umuhimu wa kijografia wa eneo hilo ndipo utawala wa Israel ukawa unatekeleza kila njama, zikiwemo za kujenga vitongoji vya Mayahudi, kubomoa nyumba za Wapalestina, kuwaua kigaidi na kubomoa nyumba zao, ili kuwafukuza katika eneo hilo na kulifanya kuwa la walowezi wa Kiyahudi. Kwa madhumuni ya kufikia lengo hilo, utawala huo tayari umefukuza makumi ya familia za Wapalestina katika mtaa huo na kutishia kufukuza wengine wengi katika siku zijazo. Kuhusu ukandamizaji huo dhidi ya Wapalestina, Mohammad Shtayyeh, Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema kwamba matukio ya Quds na Sheikh Jarrah, ni mfano mpya wa siasa zinazotekelezwa kimfumo kwa ajili ya kuwafanya Wapalestina kuwa wakimbizi.

Wapalestina wanatetea haki

Katika kukabiliana na jinai hizo za utawala wa kibaguzi wa Israel, Wapalestina wamelazimika kutetea haki zao kwa kila njia inayowezekana na hasa ya mapambano na kusimama imara mbele ya hujuma ya utawala huo. Khaled Qaddoumi, mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS mjini Tehran, anasema ghasia za karibuni ambazo zimechochewa na Israel zimewapalekea wakazi wa Kipalestina wanaoishi katika mji wa Quds kuhisi kwamba maisha yao yamo hatarini. Kwa msingi huo mtaa wa Sheikh Jarrah umebadilika kuwa nembo ya mapambano dhidi ya utawala wa Israel na Wapalestina hawana budi ila kusimama mbele ya hujuma ya wanajeshi wa utawala huo.

Uchaguzi wa Palestina

Sababu nyingine ambayo imepelekea kuibuka mapagano ya karibuni huko Quds ni uchaguzi wa Wapalestina. Uchaguzi wa Bunge la Palestina ulikuwa umempangwa kufanyika tarehe 22 ya mwezi huu wa Mei. Wapalestina wanasisitiza kufanyika uchaguzi mkuu katika mji wa Quds katika hali ambayo utawala wa Tel Aviv unapinga vikali kufanyika uchaguzi wa Wapalestina katika mji huo umbao unauchukilia kuwa ni wake. Ili kuzuia uchaguzi usifanyike utawala wa Israel umeamua kutumia mbinu ya vitisho na kuwafukuza Wapalestina katika makazi yao jambo ambalo limezua ghasia na mapigano katika mji huo. Kwa hatua hiyo utawala wa Israel unataka kuimarisha udhibitiwake wake katika mji wa Quds, udhibiti ambao ulichangiwa pakubwa na hatua iliyo kinyume cha sheria za kimataifa ya Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani ambaye aliamuru kuhamishiwa ubalozi wa nchi hiyo katika mji huo.

Siku ya Quds

Sababu ya tatu ya mapigano ya karibuni ya Quds ni maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds, siku ambayo ni ya kutetea malengo matukufu ya Palestina. Kila mwaka Wapalestina huadhimisha na kuipa umuhimu mkubwa siku hiyo ya kutetea Beitul Muqaddas na Msikiti wa al-Aqsa. Katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, Wapalestina walikuwa wamekusanyika katika msikiti huo kwa ajili ya kutetekelza ibada za mwezi huu na vile vile kulaani jinai za Israel ambapo askari wa utawala huo walivamia na kuwapiga kikatili.

Nukta ya mwsiho ni kwamba kimya cha jamii ya kimataifa kuhusu jinai za mara kwa mara za Israel dhidi ya Wapalestina zikiwemo za kubomoa na kuwafukuza kwenye makazi yao kimeufanya utawala huo umee pembe na kutekeleza jinai zaidi dhidi ya watu hao wasio na hatia.

3474654

captcha