IQNA

Wataalamu wa kimataifa katika mahojiano na IQNA

Ukatili Afghanistan unatoa kisingizio cha kuwepo wanajeshi ajinabi

12:32 - May 11, 2021
Habari ID: 3473897
TEHRAN (IQNA)- Wataalamu wa masuala ya Afghanistan wanasema Marekani na waitifaki wake hawataki kuondoka Afghanistan na wanataka kuibua hofu na wahka ili watu wa nchi hiyo wadhani kuwa bila kuwepo wanajeshi hao ajniabi mauaji yatazidi.

Weledi hao wanasema kuwa lengo jingine la mauaji yaliyokithiri Afghansitan siku za hivi karibuni ni kuidhoofisha serikali ya Afghanistan kwa maslahi ya kundi la Taliban.

Katika hujuma ya kigaidi ya Jumamosi wasichana 85 na wazazi wao waliuawa shahidi wakiwa katika ibada ya saumu na kujeruhiwa wengine zaidi ya 160. Bado maafa kamili yaliyosababishwa katika jinai hiyo hayajaweza kubainika.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Afghanistan imeitaja hujuma hiyo kuwa jinai ya kivita kwani maeneo ya elimu hayapaswi kulengwa.

Taarifa hiyo imesema kundi la Taliban limetekeleza hujuma hiyo kwa lengo la kushiniza serikali na watu wa Afghanistan.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Afghanistan amesema hata kama kundi la Taliban halijatangaza kuhusika na hujuma hiyo lakini waliokamatwa kufuatia shambulio hilo wana uhusiano na Taliban.

Kuhusiana na hujuma hiyo, mwandishi wa IQNA amezungumza na  Ali Wahidi mtaalamu wa masuala ya Afghanistan na Marvin G Weinbaum mkurugenzi wa Kituo cha Afghanistan na Pakistan katika Taasisi ya Utafiti wa Mashariki ya Kati nchini Marekani.

هدف خشونت‌ها تضعیف دولت افغانستان است

Ali Wahidi amesema katika kujibu swali la sababu za kuongezeka hujuma katika vituo vya kieleimu kama vile shle na vyuo vikuu nchini Afghanistan hasa vituo ambavyo vinamilikiwa na Waislamu wa madhehebu ya Shia amesema: "Mashambulizi hayo hayalengi eneo maalumu na ni mashambulizi ambayo ni dhidi ya binadamu na ubinadamu na yanajiri maeneo yote ya Afghansitan. Aghalabu ya maeneo yaliyolengwa ni ya Kishia".

Huku akiashiria njama ya Wamagharibi katika kuibua machafuko na ukosefu wa usalama Afghansitan amesema: "Kwa mtazamo wangu Marekani na nchi za Magharibi ziko nyuma ya pazia ya mashambulio hayo ambayo yanafanyika kwa ushirikiano wa baadhi ya tawala za kieneo zipingazo mabadiliko kama vile Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu." Amesema Marekani na waitifaki wake hawataki kuondoka Afghanistan na hivyo wanatekeleza njama ya kuibua hofu na wahka nchini humo ili wawe na kisingizio cha kubakia nchini humo.

Kuhusu uwepo wa magaidi wa ISIS au Daesh nchini Afghansitan amesema Marekani imeingiza magaidi hayo katika nchi hiyo ili wavuruge usalama ili kuwpeo kisingizio cha kubakia wanajeshi ajinabi Afghanistan. Aidha amesema kundi hilo la ISIS linapata himaya ya Marekani na baadhi ya tawala za Kiarabu kwa lengo la kuulinda utawala wa Kizayuni na kudhoofihsa nchi za eneo.

هدف خشونت‌ها تضعیف دولت افغانستان است

Halikadhalika amekosoa kimya cha jamii ya kimataifa kufuatia kuuawa shahidi makumi ya watoto wa shule nchini Afganistan. Aidha amesema shambulizi hilo la Jumamosi lililenga kuibua hitilafu za kimadhehebu na kikaumu nchini Afghanistan.

هدف خشونت‌ها تضعیف دولت افغانستان است

Kwa upande wake, Marvin G Weinbaum  mkurugenzi wa Kituo cha Pakistan na Afghanistan katika Taasisi ya Utafiti wa Mashariki ya Kati nchini Marekani katika mahojiano na IQNA kuhusu ongezeko la mashambulizi dhidi ya raia hasa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Afghanistan amesema lengo la hujuma hizo ni kuwafanya Waafghani wapoteze imani kuhusu serikali yao. Amesema magaidi wa ISIS na Taliban wamekuwa wakiwashambulia Mashia kwa muda mrefu.

Aidha amesema serikali ya Afghanistan haina uwezo wa kusitisha mashambulizi ya kigaidi nchini humo huku akitahadahrisha kuwa yamkini nchi hiyo ikatumbukia katika vita vya ndani.

/3970775

captcha