IQNA

Israel yaua Wapalestina 87 wakiwemo watoto katika hujuma Ghaza

20:16 - May 13, 2021
Habari ID: 3473905
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Afya ya Ukanda wa Ghaza ilikuwa imetangaza kuwa, wananchi 87 wa Palestina wameshauawa shahidi kutokana na mashambulizi ya kikatili ya Wazayuni.

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo ikisema kuwa, watoto 18 na wanawake 8 ni miongoni mwa Wapalestina waliouawa shahidi katika siku za hivi karibuni ambapo 388 kati yao wamejeruhiwa, 115 kati ya hao waliojeruhiwa katika mashambulio ya kikatili ya Wazayuni ni watoto wadogo na 50 ni wanawake.

Kwingineko, Chama cha Wazalishaji Bidhaa cha utawala wa Kizayuni kimetangaza kuwa, tangu yalipoanza mashambulizi ya makombora wanamapambano wa Palestina siku chache zilizopita hadi hivi sasa, sekta ya uzalishaji bidhaa ya Israel imeshapata hasara ya dola miliioni 160.

Chama hicho cha wazalishaji bidhaa cha Wazayuni  leo Alkhamisi kimekiri kuhusu hasara kubwa iliyosababishwa na mashambulio ya makombora ya wanamapambano wa Palesitna na kuongeza kuwa, sekta mbalimbali za uchumi wa Israel zimepata hasara katika mashambulizi ya tangu siku tatu zilizopita ya makombora ya wanamapambano wa Palestina.

Taarifa hiyo imesema pia kuwa, wanamuqawama wa Palestina wameshayapiga kwa makombora 540 maeneo mbalimbali ya kiuchumi ya Israel katika kipindi cha siku tatu zilizopita na kuusababishia utawala huo katili hasara ya dola milioni 160.

Kwingineko, gazeti la Marekani la Washington Post limeashiria mashambulio na jinai za hivi karibuni za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina katika mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem) na kusema kuwa sio utawala huo tu ndio unazuia kufikiwa lengo lao tukufu la kuwa na nchi huru bali Marekani pia imekuwa na mchango mkubwa katika masaibu na matatizo ambayo yamewasibu kwa miongo kadhaa sasa.

Gazeti hilo limesema kuhusu hujuma ya karibuni ya utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya Wapalestina katika mji mtakatifu wa Quds kwamba jambo la kuzingatiwa kuhusu hujuma hiyo ni msimamo wa serikali ya Rais Joe Biden ambayo imezitaka pande mbili 'kujizuia na kupunguza mivutano' na wakati huo huo kulaani mashambulio ya maroketi ya Hamas na Jihadul Islami na kutetea eti haki ya Israel 'kujilinda.'

3971438/

Kishikizo: palestina ghaza israel
captcha