Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA Afrika Mashariki, tarjama hiyo imechukua miaka saba kutayarishwa na imechapishwa na taasisi ya Al-Itrah Foundation yenye makao yake mjini Dar-es-Salaam.
Mtarjumi wa Nahj-ul-Balagha kwa lugha ya Kiswahili ni mwanazuoni maarufu wa Kiislamu Tanzania Sheikh Harun Pingili ambaye ameitarjumu kwa Kiswahili kutoka Kiarabu.
Nahj-ul-Balagha ni majmua ya khutba, barua, risala, mawaidha na semi za Amirul Muuminin Ali Bin Abu Talib AS. Majmua hiyo ilikisanywa na al-Sharif al-Radhii, mwanazuoni wa Kisia wa karne ya 10. Mbali na faida na thamani yake kubwa ya kidini, Nahj-ul-Balagha pia inasifika kwa umahiri wake wa kifasihi.
1423462