IQNA

Mabunge ya Uhispania, Ufaransa kupiga kura kuitambua Palestina

20:42 - November 14, 2014
Habari ID: 1473023
Mabunge ya Uhispania na Ufaransa yamepanga kupigia kura azimio la kulitambua taifa la Palestina, hatua ambayo imekuwa ikichukuliwa ma nchi kadhaa za Ulaya.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa  Laurent Fabius amesemanchi yake inakaribia kukamilisha mkondo wa kisheria wa kulitambua taifa la Palestina. Nchini Uhispania pendekezo la kulitambua taifa la Palestina limewasilishwa na chama cha upinzani cha kisoshalisti na utapigiwa kura na wabunge siku ya Jumanne ijayo. Inatazamiwa pia mpango huo utaungwa mkono na chama tawala cha kihafidhina. Wakati huo huo bunge la Ufaransa nalo limepanga kupiga kura kama hiyo hapo tarehe 28 ya mwezi huu kwa lengo la kulitambua taifa la Palestina. Hadi sasa nchi kadhaa zikiwemo Uingereza, Ireland na Sweden zimekwishapiga kura kama hiyo. Kura hizo zimeikasirisha mno Marekani na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel. Akikosoa uingiliaji wa Marekani kuhusu hatua hiyo, Margot Wallström, Waziri wa Mambo ya Nje wa Sweden alisema: "Marekani haipaswi kujifanya kuwa mwamuzi na mpangaji wa siasa zetu."…/mh

1473014

captcha