Matembezi hayo yalishirikisha watoto 700 wa Kipalestina ili kusisitiza umuhimu wa kufundisha watoto Quran.
Watoto hao walioshiriki ni wale ambao wamehifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu au wamehifadhi nusu ya Qur’ani Tukufu.
Matembei hayo yalianzia mbele ya Msikiti wa Al-Farouq hadi kufikia Mtaa wa Salahaddin ambapo watoto walitembea katika barabara za Kambi ya Nuseirat, wakiwa wamebeba Misahafu na mabango.
Katika hotuba baada ya kumalizika hafla hiyo, Abdul Rahman Al-Jamal, rais Taasisi ya Dar Al-Quran na Al-Sunnah ya Ukanda wa Ghaza, aliwashukuru washiriki wa matembezi hayo.
Akisisitiza kuwa watoto walioshiriki katika matembezi hayo ni "kizazi cha ukombozi" ambacho kitakomboa Msikiti wa Al-Aqsa unaokaliwa kwa mabavu na Israeli mjini Quds (Jerusalem), Al-Jamal alisema kuwa maelfu ya watoto katika Ukanda wa Gaza wanafanya kila wawezalo kuhifadhi Qur’ani.
Al-Jamal pia aliwataka wazazi kuwapeleka watoto wao katika vituo vya kidini ili waweze kuhifadhi Qur'ani Tukufu.