Jumla ya vijana 120 waliohifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu na Hadithi walihitimu katika sherehe iliyofanyika Ijumaa.
Miongoni walioshiriki katika mahafali hiyo ni maafisa wa serikali na familia za wanafunzi waliohitimu.
Akizungumza katika mahafali hiyo, Sheikh Muhammad Murad, afisa mwandamizi wa Kituo cha Qur’ani Tukufu cha Al Sidra amewapongeza wanafunzi waliohitimu kutokana na mafanikio yao makubwa.
Naye mkuu wa Kituo cha Ghaza cha Sunna na Qur’an Sheikh Marwan Aburas amesema Wapalestina katika Ukanda wa Ghaza wana uzoefu mzuri katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu na wanaweza kuwapa wengine uzoefu huo.