IQNA

Ibada ya Hija

Mahujaji wa kigeni wahudhuria mahafali ya Qur’ani ilizoandaliwa na Iran mjini Makka

22:02 - July 17, 2022
Habari ID: 3475513
TEHRAN (IQNA) – Ofisi ya Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Masuala ya Hija imeandaa mahafali za qiraa ya Qur’ani Tukufu katika mji mtakatifu wa Makka.

Mahujaji kutoka nchi mbalimbali kama Tanzania, Nigeria, Pakistan, India na Uturuki walihudhuria hafla hiyo ya Qur'ani.

Ilijumuisha visomo vya Qur’ani Tukufu ya wajumbe wa msafara wa Qur'ani wa Iran katika Ibada ya Hija, unaojulikana kama Msafara wa Nur.

Akihutubia hafla hiyo, Hujjatul Islam Ali Khayyat, naibu wa ofisi hiyo, alisisitiza nuru ing'aayo ambayo usomaji Qur’ani huibua hutokeza.

Amesema imependekezwa kuwa Waislamu wasome Qur’ani Tukufu sio tu misikitini na programu hizo za Qur'ani bali hata nyumbani.

Aidha amebaini kwamba ikiwa Hija ya Mwislamu itakubaliwa, nuru yake hukaa naye kwa muda wa miezi minne, isipokuwa itafifia kwa sababu ya madhambi.

Abolfazl Khampichi, Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa wa ofisi hiyo pia alizungumza katika hafla hiyo na kusisitiza kuwa kufanya programu hizo kunasaidia kuzima propaganda za maadui zinazolenga kuzusha mifarakano baina ya Waislamu.

 
 

4071308

 

captcha