Duru za habari zinadokeza kuwa Wizara ya Wakfu ya Kuwait imezidisha juhudi zake za kujenga mazingira ya imani na kuhakikisha waumini wana utulivu na usalama katika misikiti zaidi ya 1,590 nchini humo. Waziri wa Wakfu Abdulaziz Al-Majed amesisitiza wakati wa mkutano wake na maafisa wa wizara yake wiki iliyopita kuhusu hitajio la juhudi za pamoja, na kuwataka wakurugenzi wa misikiti katika majimbo sita kufanya usalama wa waumini na utulivu kuwa vipaumbele vyao kuu.
Vyanzo hivyo vilieleza kuwa taratibu maarufu zaidi zitakazotumika kulinda misikiti wakati wa Ramadhani ni kuzuia ombaomba, kudhibiti ukusanyaji wa michango kwa taratibu zilizoidhinishwa na Wizara ya Masuala ya Kijamii, kulinda magari ya waumini dhidi ya wizi, na kudhibiti msongamano wa magari mbele ya misikiti.
Aidha imedokezwa kuwa, Wizara ya Wakfu itaomba msaada wa wasomaji Qur'ani Tukufu kutoka nje ya nchi mwaka huu, pamoja na kuruhusu kuandaliwa futari misikiti kwa sharti kuwa futari iandaliwe katika uwanja wa msikiti na si ndani.
3482469