IQNA

Wanaharakati wafichua

Kanisa lapotosha historia ya Kiislamu katika Cordoba ya Uhispania

15:46 - March 02, 2023
Habari ID: 3476644
TEHRAN (IQNA)-Wanaharakati wameshutumu Kanisa Kikatoliki huko Cordoba, Uhispania, kwa kuharibu na kupotosha historia ya Kiislamu katika eneo hilo.

Ukosoaji huo umekuja baada ya kituo kipya cha wageni katika Kanisa Kuu Our Lady of the Assumption kupuuza au kudunisha matumizi ya zamani ya jengo hilo kama msikiti.

Ripoti ya Demetrio Fernandez, askofu wa Cordoba, ilidai  kuwa eti jengo hilo lilikuwa la Kikristo kabla ya kugeuzwa kwake kuwa Msikiti Mkuu wa Cordoba.

Mapema mwezi huu, serikali ya Uhispania ililitambua rasmi kanisa kuu hilo kuwa mali ya Kanisa Katoliki la Roma, kufuatia mijadala ya miaka mingi kuhusu mustakabali wake, ikiwa ni pamoja na matakwa ya makundi ya Waislamu wa eneo hilo kulitumia kwa Sala.

Gazeti la Kihispania El Pais lilichapisha ripoti ya Fernandez, na mipango ya Kanisa Katoliki kuhusu jengo na kusema kali ya Fernandez ni ya, “kichokozi dhidi ya utambulisho usiopingika na ulio wazi wa Kiislamu wa jengo lote hilo.”

Jose Miguel Puerta, profesa wa historia ya sanaa katika Chuo Kikuu cha Granada, aliliambia gazeti la Times: "Ni vizuri kuthamini na kuangazia historia ya Kiyahudi au za Kikristo za Cordoba, lakini hilo lisifanyika kwa kuficha utambulisho wa Kiislamu Uislamu. Haiwezekani kufuta utambulisho wa Kiislamu kwani utambulisho huu ndio fahari ya jiji.”

Kundi la wanaharakati wa Plataforma Mezquita-Catedral, wakati huo huo, limesema askofu huyo "anadunisha" historia ya Waislamu katika jengo hilo.

3482672

captcha