iqna

IQNA

syria
Misaada kwa Syria
TEHRAN (IQNA)- Shehena ya tano ya misaada ya kibinadamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa watu waliokumbwa na mitetemeko ya ardhi nchini Syria iliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Damascus mapema leo Alhamisi.
Habari ID: 3476537    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/09

Rais Assad wa Syria
TEHRAN (IQNA)- Rais Bashar al-Assad wa Syria amefichua kuwa Marekani inatoa mashinikizo kwa nchi zinazotaka kuwasaidia waathirika wa mitetemeko ya ardhi nchini Syria. Assad ameyasema hayo katika mkutano na ujumbe wa mawaziri kadhaa wa Lebanon.
Habari ID: 3476535    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/09

Zilzala Syria na Uturuki
TEHRAN (IQNA)- Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametangaza hali ya dharura katika mikoa 10 iliyotikiswa na mitetemeko miwili ya ardhi ambayo imepelekea zaidi ya watu 5,100 kupoteza maisha nchini Uturuki na Syria.
Habari ID: 3476524    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/07

Taazia
TEHRAN(IQNA)- Watu wasiopungua 2,500 wamepoteza maisha kutokana na mitetemeko miwili mkubwa ya ardhi iliyoyakumba maeneo ya kusini mashariki mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria huku idadi ya wahanga wa janga hilo ikiongezeka kila sekunde kutokana na mamia ya watu kufunikwa na vifusi vya majengo yaliyoporomoka.
Habari ID: 3476519    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/02/06

TEHRAN (IQNA) – Baraza la Fatwa la Syria limetangaza kuwa ni haramu kwa mujibu wa sheria za Kiislamu kwa Wa syria kuhatarisha maisha na mali zao kwenda Ulaya.
Habari ID: 3476083    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/11/13

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jioni ya jana ​​(Jumanne) alifanya mazungmzo na Rais Vladmir Putin wa Russia na ujumbe aliofuatana nao hapa mjini Tehran, ambako amelitaja suala la Syria kuwa muhimu sana na kusema: Suala jingine muhimu katika kadhia ya Syria ni uvamizi wa Wamarekani na kukaliwa kwa mabavu ardhi zenye rutuba na zenye utajiri mkubwa wa mafuta za mashariki mwa Furati (Euphrates), na suala hili linapaswa kupatiwa ufumbuzi kwa kufukuzwa Wamarekani kwenye eneo hilo.
Habari ID: 3475519    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/20

Kiongozi Muadhamu katika mkutano na Rais wa Uturuki
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza ulazima wa kulindwa ardhi yote ya Syria na kusema: Shambulio lolote la kijeshi katika eneo la kaskazini mwa Syria litazidhuru Uturuki, Syria na eneo zima na Asia Magharibi na kuwanufaisha magaidi.
Habari ID: 3475517    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/19

Idul Adha
TEHRAN (IQNA) - Rais wa Syria Bashar al-Assad alishiriki katika sala ya Idul-Adha huko Aleppo Jumamosi.
Habari ID: 3475481    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/07/09

Sayyid Hassan Nasrallah
TEHRAN (IQNA)- Sayyid Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amehutubu kwa munasaba wa kukumbuka kuuawa shahidi Sayyid Mustafa Badruddin na kusema kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina kulikuwa ni pigo kwa nchi za Kiarabu na mataifa yote ya eneo.
Habari ID: 3475271    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/20

Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran
TEHRAN (IQNA)- Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema kuwa, safari za hivi karibuni ya Rais Bashar al-Assad wa Syria na Amir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani nchini Iran zilikuwa za kimkakati na muhimu.
Habari ID: 3475244    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/13

Kiongozi Muadhamu katika mkutano Rais Bashar al Assad wa Syria na ujumbe alioandamana nao
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kusimama kidete taifa na serikali ya Syria na kuibuka mshindi katika vita vikubwa vya kimataifa kumeandaa mazingira ya kupata hadhi na kuheshimika zaidi nchi hiyo duniani.
Habari ID: 3475224    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/05/08

TEHRAN (IQNA)- Bibi Zainab SA alizaliwa 5 Jamadi Ula mwaka wa 5 Hijria Qamaria mjini Madina na wazazi wake ni Imam Ali AS na Bibi Fatima Zahra SA.
Habari ID: 3474933    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/02/16

Rais wa Iran
TEHRAN (IQNA)- Rais Ibrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo hapa mjini Tehran na Faisal Mekdad, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria na kusema kuwa, nchi hiyo ya Kiarabu ipo mstari wa mbele katika mapambano na muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Habari ID: 3474648    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/12/07

TEHRAN (IQNA)- Televisheni ya taifa ya Syria imetangaza kuwa askari 14 wa jeshi la nchi hiyo wameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulio la bomu lililolenga basi lililokuwa limebeba askari hao mapema leo.
Habari ID: 3474449    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/10/20

TEHRAN (IQNA)- Hujjatul Islam Sayyid Muhammad Javad Mousavi Darchei, qarii na mwalimu wa Qur’ani nchini Iran akiwa safarini nchini Syria alitembelea kaburi la Bilal Habashi , Radhi za Mwenyezi Mungu Ziwe Juu Yake, na akiwa hapo akapata taufiki ya kuadhini.
Habari ID: 3474312    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/19

TEHRAN (IQNA)- Rais Bashar al Assad wa Syria amefanya safari ya ghafla nchini Russia na kukutana na kufanya mazungmzo na Rais Vladimir Putin wa nchi hiyo katika Ikulu ya Kremlin.
Habari ID: 3474296    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/09/15

TEHRAN (IQNA)- Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imesema, shambulio la karibuni la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Syria ni uchokozi na uvamizi wa waziwazi dhidi ya ardhi ya nchi hiyo na ardhi ya Lebanon.
Habari ID: 3474121    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/07/23

Balozi wa Syria nchini mjini Tehran
TEHRAN (IQNA)- Balozi wa Syria nchini mjini Tehran amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa nchi yenye nafasi muhimu zaidi katika eneo na pia katika sera za kimataifa na inahusika katika kuibua mfumo mpya ya kimataifa.
Habari ID: 3473976    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/06/03

TEHRAN (IQNA)- Rais nchini Syria Rais Bashar al Assad kwa mara nyingine amechaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo na baada ya kutangazwa ushindi wake, wananchi wa maeneo mbalimbali ya Syria wamemiminika mitaani kusherehekea ushindi.
Habari ID: 3473953    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/28

TEHRAN (IQNA)- Rais Bashar al Assad wa Syria amejiunga na mamillioni ya Wa syria katika kupiga kura katika uchaguzi wa rais nchini humo.
Habari ID: 3473948    Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/26