IQNA

Waislamu Ulaya

Waislamu mjini Madrid wapata ardhi ya makaburi yao

20:07 - July 30, 2022
Habari ID: 3475559
TEHRAN (IQNA) - Halmashauri ya Jiji la Madrid imekubali kutenga ardhi katika mji mkuu wa Uhispania kwa ajili ya ya mazishi ya Waislamu.

Maysoun Douas, diwani wa kwanza na pekee Muislamu katika Baraza la Jiji la Mas Madrid, alitoa hotuba kuangazia matatizo na ukosefu wa haki unaoikabili jamii ya Waislamu katika eneo hilo.

Uhuru wa kidini ni pamoja na haki ya kupata maziko ya heshima bila ubaguzi kwa misingi ya kidini, alisema.

Walakini, kwa sasa kuna eneo moja tu la makaburi ya Waislamu katika eneo la Grinon jijini Madrid.

Mnamo 2016, eneo hilo lilikuwa tayari limejaa na hata kabla ya kujaa wakuu wa manispaa hawakuruhusu hata mazishi kulingana na ibada ya Kiislamu, kwa sababu sheria za manispaa zinahitaji matumizi ya jeneza.

Nafasi hiyo ilitengwa kwa ajili ya kikosi cha gadi ya Franco "Guardia Mora".

Kwa mkoa wa Madrid una takriban makaburi 250 ya umma, 14 kati ya hayo ni manispaa katika jiji la Madrid.

Kati ya makaburi hayo yote, ni eneo mmoja tu katika Grinon ambalo limetengwa kwa ajili ya Waislamu, kwa ajili ya jamii ya watu takribani 300,000 katika mkoa na 100,000 katika mji mkuu ambao wanafuata Uislamu.

Douas amesema hali hiyo inamaanisha  Waislamu wanabaguliwa na kuongeza "Wapatanishi rasmi wa masuala ya kidini, mashirika tuliyoyaamini, walituaminisha kwamba tutapata haki zetu wakati kwa hakika walikuwa wanaziteka nyara."

"Hili ni kundi linalohitaji msaada wa kitaasisi, kwani mashirika yamefanya kidogo au hayajafanya chochote kutekeleza haki za kimsingi zinazotambuliwa kwa raia wengine," aliongeza.

Inafaa kuashiria hapa kuwa Uhispania na Ureno ni nchi zilizokuwa zinatawaliwa na Waislamu kati ya miaka 711 and 1492 wakati huo eneo hilo likijulikana kama Al-Andalus. Katika karne ya 8 na 9 polepole sehemu kubwa ya Wakristo walipokea Uislamu uliokuwa dini tawala. Mnamo mwaka 1100 takriban 80% za wakazi walikuwa Waislamu.

3479900

captcha