IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Bint Maktoum yanaanza UAE

17:08 - January 08, 2024
Habari ID: 3478165
IQNA - Mashindano ya 24 YA Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind Bint Maktoum katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) yalianza Jumamosi jioni.

Mashindano ya Qur'ani yanafanyika Dubai katika vitengo tofauti kwa wanaume na wanawake.
Akihutubia hafla ya ufunguzi, mkuu wa jopo la waamuzi, Ibrahim Jassim al-Mansouri, alipongeza kuinuliwa kwa kiwango cha mashindano hayo mwaka huu, akisema ni matokeo ya maendeleo ya vituo vya kuhifadhi Qur'ani na mashindano ya ndani ya ya UAE ya Qur'ani.
Amesema kuwa takriban robo karne imepita tangu kuanza kwa mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani na hivi leo yamefikia kiwango kizuri cha ubora na wingi.
Pia alitoa wito kwa wajumbe wa jopo la majaji kuzingatia haki na usahihi katika tathmini yao ya washiriki.
Katika siku ya kwanza ya mashindano hayo washindani saba katika sehemu ya wanaume na saba kwa upande wa wanawake walipanda jukwaani kuonyesha vipaji na ujuzi wao.
Mashindano hayo ytaendelea hadi Januari 13 na sherehe za kufunga ambapo washindi watatangazwa kuwa tuzo zimepangwa Januari 16 kwa upande wa wanaume na Januari 17 kwa upande wa wanawake.
Mwaka huu mashindano hayo yana kategoria sita: kuhifadhi Qur'ani nzima, kuhifadhi Juzuu 20, kuhifadhi Juzuu Juzi 10, kuhifadhi Juzuu 5 ( kwa raia  wa UAE tu), kuhifadhi Juzuu 5 (kwa wakaazi chini ya miaka 10), na kuhifadhi Juzuu 3 (kwa raia chini ya miaka 10).
Mashindano ya Qur'ani Tukufu ya Sheikha Hind Bint Maktoum huandaliwa kila mwaka na Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai (DIHQA) kwa lengo la kuwaenzi wahifadhi Qur'ani hususan wanawake.

 
4192565

Habari zinazohusiana
captcha