IQNA

Maonyesho ya Kumbukumbu ya Kubomolewa Makaburi ya Baqi katika Haram ya Imam Ridha (AS)

IQNA - Maonyesho ya Kumbukumbu ya Kubomolewa Makaburi ya Baqi yamefanyika katika Haram ya Imam Ridha (AS) mnamo Aprili 17, 2024.

Tarehe 8 Shawwal mwaka 1344 Hijiria inakumbushia tukio la uharibifu mkubwa wa makaburi ya Baqi ya mjini Madina ambayo ni eneo muhimu la historia ya Waislamu. Katika mwaka huo, Mawahabi (Answar Suna) walivamia makaburi hayo na kuyabomoa huku wakipiga ngoma na kucheza. Katika makaburi ya Jannatul Baqi wamezikwa Ahul Bayt wa Mtume SAW.  Baada ya Muhammad Ibn Saud kutawala tena maeneo ya Hijaz, likiwemo eneo la Madina, Sheikh Abdullah bin Balihad mmoja wa makadhi wa Mawahabi, alitoa fatwa ya kuhalalisha kuharibiwa kwa makaburi matukufu na ya kihistoria ya mjini Madina. Mawahabi walikusanya watu kwa nguvu na kuwalazimisha kwenda katika makaburi hayo ya Baqii na kuanza kubomoa na kuharibu kila kitu kilichokuwa juu ya makaburi ya mji wa Madina na nje ya mji huo.

 
 
Kishikizo: baqii ، baqi ، madina