IQNA

Magaidi wa Daesh (ISIS) wabomoa makaburi wa mawalii Syria

17:02 - June 24, 2015
Habari ID: 3318384
Magaidi wa kundi la Kitakfiri la Daesh au ISIS wamebomoa makaburi mawili ya kale ya Mawalii wa Allah SWT katika mji wa kihistoria wa Palmyra mkoani Homs nchini Syria.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Turathi za Kale Syria, Maamoun Abdulkarim, siku tatu zilizopita magaidi hao wa Kitakfiri walilipua mabomu ndani ya majengo ya makaburi ya Mohammad bin Ali wa kizazi cha binamu yake Mtume Muhammad SAW na Nizar Abu Bahaaeddine, msomi mtajika wa Kiislamu kutoka Palmyra. Afisa huyo wa Syria amesema kuwepo maziara hayo ya Kiislamu ni kinyume cha itikadi za magaidi wa Daesh na kwa msingi huo mbali na kubomoa maeneo hayo matakatifu wanawazuia watu kuyazuru. Amesema magaidi wa Daesh tayari wameshabomoa makaburi zaidi ya 50 ya hadi miaka 200 iliyopita katika maeneo wanayodhibiti kaskazini na mashariki mwa Syria.

Nchini Iraq na Syria magaidi wa Daesh wamebomoa makaburi ya Mitume, Manabii, Masahaba Watukufu wa Mtume SAW na Mawalii wa Allah SWT.

Magaidi wa kitakfiri wa Daesh wanafuata itikadi ya Kiwahabi ambayo inapinga kuwepo kumbukumbu za Waislamu kama vile makaburi au maziara matakatifu na wanawakufirisha Waislamu wote wanaokuwa na itikadi hiyo yenye chimbuko la Kiislamu.../mh

3318001

captcha