IQNA

Maulamaa wa Iraq

Makaburi ya Janatul Baqi, Madina, yakarabatiwe

11:35 - July 25, 2015
Habari ID: 3332765
Makhatibu wa Sala ya Ijumaa nchini Iraq wametoa wito wa kukarabatiwa makaburi ya Janatul Baqi ambayo yalibomolewa na utawala wa Aal Saud.

Katika khutba zao za Ijumaa wameashiria kuharibiwa makabari ya Jannatul Baqi na kusema kitendo hicho na jinai iliyolenga kuibua mifarakano baina ya Waislamu.
Itakumbukwa kuwa siku kama ya leo miaka 92 yaani tarehe 8 Shawwal mwaka 1345 (1925) Mawahabi walibomoa makaburi ya Ahlul Bait wa Mtume SAW ambayo yako Baqii, katika mji mtakatifu wa Madina.
Baada ya Muhammad Ibn Saud kutawala tena baadhi ya maeneo ya Hijaz, ukiwemo mji wa Madina, Sheikh Abdullah bin Bulaihad aliyekuwa Kadhi Mkuu wa Kiwahabi, alitoa fatuwa ya kubomolewa makaburi matukufu na ya kihistoria ya mjini Madina.
Mawahabi walikusanya watu kwa nguvu na kuwalazimisha kwenda katika makaburi hayo ya Baqii na kuanza kubomoa na kuharibu kila kitu kilichokuwa juu ya makaburi ya mji huo na nje ya mji. Miongoni mwa makaburi yaliyobomolewa na kuharibiwa vibaya ni makaburi manne ya .maimamu na wajukuu wa Mtume SAW

Hadi leo watawala wa Saudi Arabia wanaendelea kuharibu turathi za kale za Kiislamu nchini humo kwa visingizio mbali mbali.

Mawahabi wanaotekeleza uharibifu huo wanakusudia kufuta kabisa kumbukumbu zote za historia adhimu ya Uislamu ambapo hivi sasa miji mitakatifu ya Makka na Madina inaendelea kushuhudia maeneo mengi ya historia ya Kiislamu yakimbomolewa.../mh

3332611

Kishikizo: madina baqi makaburi saud
captcha