IQNA

Maonyesho ya Qur'ani katika miji 100 kote Iran

11:41 - June 22, 2016
Habari ID: 3470410
Kunafanyika maonyesho ya Qur'ani katika miji 100 nchini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam Mohammad Ridha Heshmati Naibu Waziri wa Utmaduni na Muongozi wa Kiislamu Iran anayesimamia masuala ya Qur'ani. Akizungumza Jumanne wakati wa kufunguliwa kitengo cha kimataifa katika Maonyesho ya 24 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran amesem kuwa, mbali na Tehran, miji mingine mikubwa Iran pia huwa mwenyeji wa maoneysho ya Qur'ani Tukufu.

Amesema maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani Tehran yanafanyika katika eneo lenye ukubwa wa mita mraba 50,000 katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA. Ameongeza kuwa, pembizoni mwa monyesho hayo, kutakuwa na vikao vya kimataifa vya wataalamu wa Qur'ani Tukufu kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika nyuga mbali mbali za Qur'ani baina ya nchi za Kiislamu.

Maoneysho ya 24 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu mjini Tehran yana washiriki kutoka nchi 20 za kigeni ikiwa ni pamoja na nchi kadhaa za Ulaya, Afrika Kaskazini na nchi za Kiislamu zinazopakana na Iran.
Aidha wataalamu wa Qur'ani kutoka nchini 15 wanaoshiriki katika maonyesho ya mwaka huu.
Kati ya nchi za kigeni zinazoshiriki maonyesho ya mwaka huu ni Algeria, Uturuki, Iraq na Italia.

Maonyesho ya mwaka huu ambayo yalianza tarehe Mosi mwezi Mtukfuu wa Ramadhani na kufunguliwa rasmi tarehe 13 Juni yanatazamiwa kumalizika 30 Juni. Maonyesho hayo yana vibanda 300 huku kitengo cha vitabu kikiwa kikubwa zaidi.
Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tehran ni makubwa zaidi ya aina yake duniani.

Maonyesho hayo hufanyika kila mwaka katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Tehran ambapo huwa na vitengo kadhaa vya maudhui mbali mbali za Qur'ani.

3509330

captcha