IQNA

Kundi la Taliban lasema hujuma dhidi ya misikiti zinaetekelezwa na mashirika ya kijasusi ya maadui

19:50 - June 13, 2020
Habari ID: 3472861
TEHRAN (IQNA) - Kundi la Taliban limetoa taarifa na kusema hujuma dhidi ya misikiti nchini Afghanistan zinatekelezwa na mashirika ya kijasusi ya maadui.

Taarifa ya Taliban imesema hujuma za hivi karibuni dhidi ya misikiti, mazishi, hospitali na uharibiufu wa miundo msingi ni sehemu ya njama za maadui wanaolenga kueneza hofu na wahka ili kuvuruga mchakato wa amani nchini humo.

Taarifa hiyo imetolewa baada watu wane kupoteza maisha kufuatia hujuma ya kigaidi iliyolenga msikiti katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul siku ya Ijumaa.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghansitan imesema hujuma hiyo ilijiri wakati wa Swala ya Ijumaa katika mji wa Sher Shah Suri, magharibi mwa Kabul. Miongoni mwa waliouawa katika hujuma hiyo ya bomu ni Imamu aliyekuwa akiswalisha.Hakuna kundi lolote ambalo limekiri kuhusika na hujuma hiyo.

Kundi la kigaidi la ISIS lilidai kuhusika na hujuma ya mapema mwezi huu  iliyolenga msikiti katika eneo lenye usalama mkali ambalo aghalabu ya wakazi wake ni wanadiplomasia.

Tawkimu zinaonyesha kuwa machafuko yaliongezeka Afghanistan baada ya kufikiwa mapatano baina ya Marekani na kundi la Taliban mwezi Februari mwaka huu.

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulionya kuhusu ongezeko la mashambulizi dhidi ya raia na kutozingatiwa sheria za kibinadamu nchini Afghanistan.

3471671/

captcha