Kwa mujibu wa tovuti ya youm7, Jumuiya ya Kimataifa ya Waislamu (MWL), imemteua Sheikh Taruti kuongoza baraza hilo.
Taruti alizwaliwa mwaka 1965 katika kijiji cha Tarut karibu na mji wa Zagazig jimboni Sharqia. Alianza kuhifadhi Qur’ani akiwa na umri wa miaka mitatu na alifanikiwa kuhifadhi Qur’ani kikamilifu akiwa na umri wa miaka 8. Taruti alisoma katika tawi la Zagazig la Chuo Kikuu cha Al Azhar na aliendelea kuimarisha uwezo wake wa Qur’ani kwa kupata mafunzo kwa kutoka kwa wasomi wakubwa kama vile Sheikh Mohammad Al-Lithi, Shahat Anwar and Saeed Abdul Samad.