IQNA

Hujuma ya Marekani Afghanistan imeua raia wakiwemo watoto

19:25 - August 30, 2021
Habari ID: 3474239
TEHRAN (IQNA)- Watoto wadogo ni miongoni mwa raia kadhaa waliouawa katika shambulio la ndege isiyo na rubani ya Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kabul, mji mkuu wa Afghanistan.

Duru za habari Kabul zinasema

watoto watatu ni miongoni mwa raia wasiopungua sita waliouawa katika hujuma hiyo ya drone ya Marekani.

Baadhi ya duru za habari zimearifu kuwa, watu tisa wa familia moja wakiwemo watoto sita ndio waliouawa katika shambulio hilo la jeshi la Marekani, eti la dhidi ya gari lililokuwa limesheheni mada za miripuko karibu na Uwanja wa Ndege wa Kabul.

Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTOM) sambamba na kukiri kuwa raia kadhaa ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulio hilo, lakini inasisitiza kuwa hujuma hiyo ya droni imeua magaidi kadhaa waliokuwa wamejifunga mada za miripuko, wakijiandaa kwenda kujiripua katika Uwanja wa Ndege wa Kabul. 

Kundi la Taliban ambalo sasa linatawala Afghanistan limelaani vikali hujuma hiyo ya Marekani.Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid amesema iwapo Marekani ilihisi kuna hatari katika jengo lililolengwa ingepaswa kujulisha Taliban na kuongeza kuwa hatua hiyo ya Marekani ilikuwa ni kinyume cha sheria.

Kabla ya hapo pia, askari wa Marekani walituhumiwa kuua raia katika shambulio la Kabul la Alkhamisi ya wiki iliyopita. Watu wasiopungua 175 wakiwemo askari 13 wa US waliuawa na wengine kadhaa walijeruhiwa kufuatia miripuko miwili ya mabomu iliyotokea nje ya Uwanja wa Ndege wa Hamid Karzai mjini Kabul nchini Afghanistan.

Kundi la kigaidi la ISIS lilitangaza kuhusika na hujuma hiyo ambayo ni ya kwanza kutokea mjini Kabul tangu rais Ashraf Ghani aitoroke nchi; na mji mkuu huo wa Afghanistan kudhibitiwa na kundi la Taliban mnamo tarehe 15 Agosti.

3475587

Kishikizo: kabul taliban
captcha