IQNA

Kiongozi wa Hamas aishukuru Iran kwa kuunga mkono ukombozi wa Palestina

13:47 - September 05, 2021
Habari ID: 3474259
Kiongozi wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuendelea kuunga mkono Wapalestina na harakati zao za muqawama au mapambano.

Ismail Haniya, kiongozi wa Idara ya Kisiasa ya Hamas ameyasema hayo wakati alipompigia simu Hossein Amir-Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na kumpongeza kufuatia kuteuliwa kushika wadhifa huo.  Haniya amesema Wapalestina wanatoa shukrani zao za dhati kutokana na msimamo wa Iran wa kuunga mkono harakati za ukombozi wa Palestina.

Kwa upande wake, Amir-Abdollahian amewapongeza wanamapambano wanaume na wanawake wa Palestina kutokana na mapambano yao dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel hasa mapambano yao hivi karibini ya vita vya siku 11 mwezi Mei wakati utawala huo ghasibu ulipotekeleza mashambulizi mutawalia dhidi ya Ukanda wa Ghaza.

Aidha amesema njia pekee ya Wapalestina kukomboa ardhi zao zinazokaliwa kwa mabavu na Israel ni kupitia mapamabano . Amir-Abdollahian amesema: “Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, sawa na miaka ya nyuma, inaunga mkono mapambano ya kukombolewa ardhi zote za Palestina na kuundwa nchi huru ya Palestina katika ardhi zote zake za kishitoria na mji mkuu wake ukiwa ni Quds (Jerusalem).”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia amelaani vikali muendelezo wa jinai za Israel dhidi ya wanawake na watoto Wapalestina. Amesema Iran inaunga mkono suluhisho la kisias ala kadhia ya Palestina kupitia kura ya maoni ya wakaazi asili wa Palestina ambao wataainisha hatima yao wenyewe.

3475626

captcha