IQNA

UNESCO yatambua kaligrafia ya Kiislamu kuwa turathi ya kimataifa

16:23 - December 17, 2021
Habari ID: 3474684
TEHRAN (IQNA)- Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeongeza kaligrafia ya Kiislamu na Kiarabu katika orodha yake ya mwaka 2021 ya Turathi za Kiutamaduni za Mwanadamu.

Uamuzi huo wa UNESCO umekuja baada ya pendekezo la nchi 15 za Kiislamu ambazo mwaka ujao zitawasilisha ripoti zikibainisha hatua zilizochukuliwa kuimarisha sanaa hiyo ya kaligrafia ya Kiislamu na Kiarabu.

Kaligrafia ya Kiarabu ni mtindo wa kipekee wa kuandika maandish ya Kiarabu yenye mvuto wa aina yake.   

Orodha ya  Turathi za Kiutamaduni za Mwanadamu ilianzishwa mwaka 2008 na hujumuisha masuala ya kiutamaduni. Katika miaka ya hivi karibuni orodha hiyo imejumuisha mizik, densi, michezo na tamasha na pia vyakula.

3476962

Kishikizo: kaligrafia
captcha