Rais Ebrahim Raisi alisema hayo Jumatano, muda mfupi baada ya kutokea shambulio hilo la kigaidi lililoua na kujeruhiwa makumi ya watu. Rais wa Iran amesisitiza kuwa: Shambulio hilo la kikatili halitapita hivi hivi bila ya kujibiwa.
Sayyid Ebrahim Raisi ameeleza bayana kuwa, "Vikosi vya usalama na sheria vya nchi hii baada ya kutambua mzizi wa jinai hiyo ya kihaini, vitatoa jibu mwafaka kwa wapangaji na watekelezaji (wa jinai hiyo)."
Ameeleza kuwa, "uzoefu unaonesha kuwa, maadui wa Iran wanalipiza kisasi kwa kufeli njama zao za kuibua migawanyiko miongoni mwa jamii zilizoshikamana za Wairani."
Rais Raisi amesema maadui wa Jamhuri ya Kiislamu hivi sasa wamegeukia mbinu za ghasia na ugaidi kujaribu kukwamisha ustawi na maendeleo hapa nchini.
Watu wasiopungua 15 wameuawa huku 27 wakijeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi la jana Jumatano mwendo wa saa 12 kasorobo kwa saa za hapa nchini, katika Haram Tukufu ya Shah Cheragh mjini Shiraz, katika mkoa wa Fars kusini magharibi mwa nchi.
4094764