Kituo cha Imam Hussein (AS) cha mjini Tiro kiliandaa hafla hiyo kabla ya mwaka wa tatu wa kuuawa shahidi makamanda hao.
Ilihudhuriwa na watu mashuhuri wa kidini kama Sheikh Ali Arif na Hajj Bilal Daghir pamoja na maafisa kadhaa wa Hizbullah.
Maqari kadhaa, akiwemo Abdul Rahman al-Khouli kutoka Misri na Mohammad Ghalmoush kutoka Lebanon, walikariri aya za Qur'ani Tukufu katika ibada hiyo ya kumbukumbu.
Pia iliangazia hotuba za watoto kadhaa wa mashahidi wa Hizbullah na kuonyeshwa klipu ya video kuhusu Jenerali Soleimani.
Lt. Jenerali Soleimani, ambaye alikuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Naibu Kamanda Jeshi la Kujitolea la Wannachi wa Iraq (PMU) Abu Mahdi al-Muhandis, na wanamapambano wenzao waliuawa katika shambulio la ndege zisizo na rubani za Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mapema Januari 3, 2020. Shahidi Soleimani alikuwa ameelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa serikali ya nchi hiyo.
Ikulu ya White House na Pentagon ilitangaza kuwa ilihusika na mauaji hayo ya kigaidi na kuthibitisha kuwa shambulio hilo lilitekelezwa kwa maelekezo ya Rais wa Marekani wa wakati huo Donald Trump.
Mipango mbalimbali imepangwa kuandaliwa nchini Iran, Iraq na nchi nyingine kadhaa ili kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kishahidi cha Jenerali Soleimani, al-Muhandi na wanajihadi wenzao.
4111031