Alikuwa miongoni mwa wasomaji wanne wa Qur'ani waliokuwa wamefika kwenye fainali ya shindano hilo la Qur'ani Tukufu.
Shahmoradi alipokea zawadi ya fedha taslimu riyal milioni tatu za Saudia au USD 800,000 kwa kuchukua nafasi ya kwanza katika kitengo cha usomaji wa Qur'ani.
Wengine watatu walioingia fainali katika kitengo hiki walikuwa Abdul Aziz Faqih kutoka nchi mwenyeji aliyemaliza mshindi wa pili na Wamorocco Zakariya al-Zirak na Abdullah Al-Dughri waliibuka wa tatu na wa nne mtawalia.
Shindano hilo liliianza siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani (Machi 23).
Waandalizi wanasema moja ya malengo yao yalikuwa ni kuangazia wingi wa tamaduni katika ulimwengu wa Kiislamu, kupitia kusoma Qur'ani Tukufu na Adhana..
Mwaka huu, shindano hilo lilivutia washiriki 50,000 Waislamu kutoka zaidi ya nchi 100, wote wakiwania kufuzu.
Kati ya washiriki 2,116 walioshinda, washiriki 36 (18 katika qiraa au usomaji Qur'ani na 18 katika adhana) walifuzu kwa hatua za mwisho.
Jumla ya pesa za tuzo za shindano hilo zilizidi riyal milioni 12 za Saudi ($ 3.2 milioni).
4132262