IQNA

Hija 1444

Mahujaji Wachina wavutia wengi baada kusafisha mitaa ya Makka kabla ya kurejea makwao

20:20 - July 15, 2023
Habari ID: 3477288
MAKKA (IQNA) - Mahujaji wa China wamepongezwa sana kwa hatua yao ya kusafisha barabara na vijia katika mji mtakatifu wa Makka (Mecca) kabla ya kurejea katika nchi yao baada ya kukamilisha ibada ya Hija mwaka huu.

Klipu iliyosambazwa kwa wingi  kwenye mitandao ya kijamii, monyesha Mahujaji wa China wakikusanya taka katika katika jiji hilo takatifu.

Ibrahim bin Ahmed Al-Ghamdi, Naibu Meya wa Makkah, aliwaalika Mahujaji hawa ofisini kwake na akawapa zawadi na nishani ya heshima.

Aliwashukuru na kuwashukuru Mahujaji Wachina kwa ubunifu wao huo, ambao alisema umesaidia kuongeza uelewa wa usafi mazingira kwa Mahujaji na kuwahimiza kuendeleza utamaduni wa usafi ili kuiweka Makka katika hali ya usafi daima..

Musa Boi Long, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Masuala ya Hijja ya China, alitoa shukrani zake kwa Saudi Arabia na mashirika yake kwa kuwahudumia Mahujaji.

Ujumbe wa kwanza rasmi wa Hija kutoka China ulikuwa mwaka 1955 na ulikuwa na Mahujaji 20 pekee. Mnamo mwaka wa 2016, China ilifikia rekodi ya idadi ya mahujaji wapatao 14,000, theluthi moja yao wakiwa wanawake kutoka mikoa tofauti ya Uchina.

3484346

Kishikizo: china Hija 1444
captcha