IQNA

Kimbunga cha Al Aqsa

Hizbullah:Israel haitanusurika katika kinamasi ilichotumbukia huko Gaza

14:58 - November 02, 2023
Habari ID: 3477830
BEIRUT (IQNA) - Israel ilianguka baada ya Harakati za Mapambano ya Kiisalmu ya Palestina kuanzisha Operesheni Kimbunga cha Al-Aqsa katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu Oktoba 7 na haitanusurika kwa njia yoyote kwenye kinamasi chake katika Ukanda wa Gaza, afisa wa ngazi ya juu wa harakati ya muqawama ya Lebanon Hizbullah alisema.

Seyyed Hashem Safieddine, Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah aliyasema hayo katika mahojiano na waandishi habari kutoka Iran katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut siku ya Jumanne.

Safieddine ameashiria ripoti na taarifa sahihi za uwanja ambazo Hizbullah iliipata tangu kuanza kwa mashambulizi ya kushtukiza ya Wapalestina na kusema: "Baada ya mafanikio ya Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa, utawala wa Kizayuni ulisambaratika kabisa katika masuala ya kijeshi na kijasusi."

Akisisitiza kwamba Hizbullah ya Lebanon haikuwa na ujuzi wa awali wa operesheni ya Palestina na imesikia kuhusu operesheni hiyo kutoka kwa vyombo vya habari, Safieddine alisema operesheni hiyo ilikuwa ya Palestina kabisa na Hizbullah ilifurahishwa na kwamba Hamas imepata uwezo huo wa juu wa kijasusi.

Akithibitisha tena kwamba jeshi la utawala ghasibu wa Israel liko katika hali mbaya zaidi na limeporomoka baada ya shambulio la tarehe 7 Oktoba.. Aidha afisa huyo wa Hizbullah amesema mifumo ya kiusalama na kijasusi ya utawala wa Kizayuni ilisambaratika katika matukio ya hivi karibuni na maafisa wake wa ngazi za juu wa kijeshi wako katika hali ya sintofahamu na kutoelewana. .

Akigusia madai kuhusu hatua ya kijeshi ya utawala wa Israel dhidi ya Iran, afisa huyo wa Hizbullah alisema, “Kwanza, ni bora wasimamishe vita vinavyoendelea na waone jinsi hali inavyoendelea baada ya vita hivyo, kisha wazungumzie kuhusu Iran. Utawala wa Kizayuni hautatoka kwenye kinamasi huko Gaza bila kudhurika."

Habari zinazohusiana
captcha