IQNA

Umrah

Ziyara katika Al-Rawdah Al-Sharifa mjini Madina itakuwa mara moja tu kwa mwaka

18:04 - December 24, 2023
Habari ID: 3478085
IQNA - Wizara ya Hija na Umrah ya Saudi Arabia imetangaza kuwa kila mwenye kushiriki katika ibada ya Hija ndogo ya Umra anaruhusiwa kutembelea Al-Rawdah Al-Sharifa katika mji mtakatifu wa Madina mara moja tu kwa mwaka.

Wizara ilisema katika taarifa kwamba kibali cha ziara hiyo kinaweza kupatikana tu kupitia programu au aplikesheni za Nusuk au Tawakkalna.

Wale ambao hawajatembelea eneo hilo hadi sasa au ambao hawajatembelea eneo hilo kwa angalau siku 365 wanaweza kupata kibali, iliongeza.

Kila Hujaji anaweza kukaa kwenye Al-Rawdah Al-Sharifa kwa dakika kumi tu, ilisema taarifa hiyo. Hatua hiyo inalenga kuwezesha waumini wote kupata fursa ya kuzuri eneo hilo takatifu. Mahujaji wa kike wanaweza kutembelea eneo hilo kila siku baada ya sala ya asubuhi hadi saa tano asubuhi na tena baada ya sala ya Isha hadi usiku wa manane, taarifa hiyo ilisema.

Mahujaji wa kiume wanaruhusiwa kutembelea eneo hilo kuanzia saa tano mchanai hadi kuanza kwa swala ya Isha, wizara iliendelea kusema.

Msikiti wa Mtume (Al-Masjid an-Nabawi) ulioko Madina ni eneo iliko Al-Rawda Al-Sharifa ambapo kaburi la Mtume Muhammad (SAW) lipo.

Baada ya kufanya ibada ya Umrah kwenye Msikiti Mkuu, eneo takatifu zaidi la Uislamu huko Makka, wengi wanaoshiriki hija hiyo ndogo humiminika kwenye Msikiti wa Mtume kuswali na kutembelea Al-Rawdah Al-Sharifa.

Saudi Arabia inatarajia Waislamu wapatao milioni 10 kutoka nje ya nchi kufanya Umrah katika msimu huu.

Msimu huo ulianza mwezi mmoja uliopita baada ya kumalizika kwa ibada ya Hija ya Kiislamu ya kila mwaka ambayo takriban Waislamu milioni 1.8 walihudhuria kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitatu baada ya vizuizi vinavyohusiana na janga kuondolewa.

4189609

Habari zinazohusiana
captcha