IQNA

Ahadi ya Kweli

Mbunge wa Uturuki asoma Qur'ani kupongeza Operesheni ya 'Ahadi ya Kweli' ya Iran dhidi ya Israel

20:25 - April 20, 2024
Habari ID: 3478706
IQNA - Mbunge mmoja wa Uturuki ameiongeza Iran kwa kutekeleza operesheni ya makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya utawala wa Israel hivi karibuni.

Mehmet Sait Yaz, mjumbe wa Chama cha Haki na Maendeleo anayewakilisha watu wa Diyarbakir, katika hotuba yake bungeni alisoma aya ya kwanza ya Surah Al-Fil ya Qur'ani Tukufu isemayo:  Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo watenda wale wenye tembo?. Ameisoma aya hiyo na kisha kutoa shukrani zake za dhati kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na kutekeleza operesheni hiyo dhidi ya utawala wa kigaidi wa Israel.

Amesema licha ya kuwa Marekani na Israel zilisema haiwezekani nchi yoyote kuthubutu kuishambulia Israel, utawala huo wa Israel  ulilengwa kwa makombora ya Iran.

Amewashukuru na kuwapongeza wananchi na serikali ya Iran kwa operesheni hiyo ya kijeshi yenye mafanikio.

Ikumbukwe kuwa Aprili Mosi utawala wa Kizayuni ulifanya shambulizi la kigaidi dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus, mji mkuu wa Syria, na kupelekea kuuawa shahidi washauri saba wa kijeshi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC)  ambao walikuwa nchini Syria kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo. Katika kujibu jinai hiyo mapema Jumapili tarehe 14 April 2024 Iran ilifanya mashambulizi ya moja kwa moja ya ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya Israel.

Operesheni hiyo ya kijeshi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliyopewa jina la Ahadi ya Kweli ilikuwa haki yake ya kimsingi ya kujilinda, ambayo imeelezwa wazi chini ya Ibara ya 51 ya Hati ya Umoja wa Mataifa na katika kukabiliana na uchokozi wa kijeshi wa mara kwa mara wa utawala wa Israel, hasa mashambulizi ya kijeshi ya utawala huo dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran, mashambulizi ambayo ni kinyume kabisa cha kifungu cha 2 ibara ya 4 ya hati hiyo.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Meja Jenerali Hossein Salami ameuonya utawala wa Israel kwamba jibu la Iran litakuwa "kali zaidi" ikiwa utawala huo utatoa jibu kwa operesheni ya kulipiza kisasi ya Iran. Salami alisisitiza kwamba Iran inaweza kufanya operesheni kwa kiwango kikubwa zaidi lakini shambulio hilo "lilikuwa na mipaka" kwa kambi za kijeshi za utawala wa Kizayuni, kutoka Miinuko ya Golan hadi Jangwa la Negev, ambazo zilitumiwa katika shambulio la kigaidi kwenye ubalozi mdogo wa Iran jijini Damascus. Iran imeuonya vikali utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa utakabiliwa na jibu kali ukijaribu kurudisha mapigo baada ya operesheni hiyo ya Iran ya kulipiza kisasi.

3488000

 

Kishikizo: Ahadi ya Kweli
captcha