iqna

IQNA

china
TEHRAN (IQNA) – Mkuu wa Shirika la Kiislamu la Haki za Binadamu (IHRC) lenye makao yake London amelaani kimya cha jamii ya kimataifa kuhusu ukandamizaji wa jamii za Waislamu waliowachache nchi mbali mbali duniani.
Habari ID: 3472989    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/07/22

TEHRAN (IQNA)- Wataalamu Wairani wamefanikiwa kuunda kifaa maalumu (test kit( cha kupima kirusi cha Corona. Kifaa hicho ni cha kwanza cha aina hiyo kuundwa nchini Iran.
Habari ID: 3472500    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/02/24

TEHRAN (IQNA) – Nakala ya kale zaidi ya Qur'ani Tukufu nchini China imewekwa katika maonyesho ya umma kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Qinghai, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Habari ID: 3472245    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/12/01

TEHRAN (IQNA) – China imetoa taarifa na kupinga madai ya kimataifa kuwa imewaweka Waislamu wa mkoa wa Xinjiang katika kambi maalumu kwa lengo la kuwabadilisha itikadi zao.
Habari ID: 3472232    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/11/26

TEHRAN (IQNA) – Shirika moja la kutetea haki a binadamu limeitaka serikali ya China kuwaachilia huru watoto Waislamu wa jamii ya Uighur wanaoshikiliwa kinyume cha matakwa ya wazazi wao katika shule za bweni za serikali mkoani Xinjiang.
Habari ID: 3472132    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/09/16

TEHRAN (IQNA)- Msikiti umebomolewa katika mkoa wa Gansu, kaskazini-kati mwak China ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya kufuta turathi za Kiislamu nchini humo.
Habari ID: 3471922    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/20

TEHRAN (IQNA) - Picha za satalaiti zinaonyesha kuwa serikali ya China inabomoa misikiti muhimu ya eneo lenye Waislamu wengi la Xinjiang.
Habari ID: 3471908    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/04/10

TEHRAN (IQNA) –Serikali ya China inaendeleza ukandamizaji wake wa jamii ya Waislamu nchini humo na sasa inatumia kamera maalumu kwa lengo la kuwachunguza na kuwadhibiti Waislamu.
Habari ID: 3471848    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/02/21

TEHRAN (IQNA)- Utawala wa China umepitisha sheria mpya ya kuufanya Uislamu nchini humo uendane na itikadi ya 'Usosholisti wa Ki china ' katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Habari ID: 3471799    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/01/07

TEHRAN (IQNA)-Wakuu wa utawala wa China wamefunga misikiti mitatu katika mji wa Weishan katika mkoa wa Yunnan kusini mwa nchi hiyo.
Habari ID: 3471795    Tarehe ya kuchapishwa : 2019/01/02

TEHRAN (IQNA) – Utawala wa China unaendelea kupuuza malalamiko ya dunia kuhusu kuendelea kuteswa Waislamu waliowachache nchini humo.
Habari ID: 3471740    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/11/13

TEHRAN (IQNA)- Utawala wa China unawatenganisha watoto Waislamu na wazazi wao ambao wanashikiliwa katika gereza au kambi maalumu za mafunzo ya Kikomunisti.
Habari ID: 3471682    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/09/21

TEHRAN (IQNA)- Wataalamu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa China kuwaachilia huru mara moja Waislamu wanaoshikiliwa katika kambi za kuwafunza Ukomunisti na kwa kisingizio cha kukabiliana na ugaidi.
Habari ID: 3471657    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/09/02

TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya Waislamu nchini China wamekusanyika katika msikiti mmoja kaskazini magharibi mwa nchi hiyo katika maandamano nadra ya kupinga mpango wa kuubomoa.
Habari ID: 3471625    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/08/11

TEHRAN (IQNA)- Wakuu wa utawala wa China wanawashikilia kwa nguvu Waislamu karibu milioni 1 katika kambi zenye msongamano mkubwa ambapo wanafunzwa kwa lazima itikadi za Kikomunisti.
Habari ID: 3471554    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/06/12

TEHRAN (IQNA)- Misitiki yote nchini China imetakiwa kupeperusha bendera ya taifa hilo katika maeeneo ya juu na muhimu ya msikiti, Jumuiya ya Kiislamu China imetangaza.
Habari ID: 3471527    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/05/22

TEHRAN (IQNA)-Jamii ya Waislamu inazidi kuongezeka huko Hong Kongo, eneo lenye mamlaka ya kujitawala nchini China, na kwa msingi huyo kumeanzishwa jitihada za kujenga msikiti mpya ambao ujenzi wake umekwama kwa muongo moja sasa.
Habari ID: 3471466    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/04/15

TEHRAN (IQNA)-Waislamu zaidi ya 100,000 kutoka jamii ya Uighur nchini China wanasemekana kushikiliwa kwa nguvu katika kambi zenye msongamano mkubwa ambapo wanafunzwa itikadi za Kikomunisti.
Habari ID: 3471373    Tarehe ya kuchapishwa : 2018/01/27

TEHRAN (IQNA)-Muislamu mmoja nchini China amehukumiwa kifungo cha miaka 16 jela baada ya kupatikana na faili za sauti (Audio) za qiraa ya Qur'ani Tukufu kwenye kompyuta yake.
Habari ID: 3471291    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/12/02

TEHRAN (IQNA)-Serikali ya China imefunga duka moja maarufu la vitabu vya Kiislamu na kumtia mbaroni mmiliki wa duka hilo kwa tuhuma za ugaidi.
Habari ID: 3471212    Tarehe ya kuchapishwa : 2017/10/11