IQNA – Maqari mashuhuri wa Qur'ani kutoka Iran wanatarajiwa kuzuru Tanzania kushiriki katika kongamano kubwa la kimataifa la Qur'ani litakalofanyika jijini Dar es Salaam.
IQNA – Maelfu ya watu wameandamana katika mitaa ya Paris na miji mingine ya Ufaransa siku ya Jumapili kulaani ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu na kumuenzi Aboubakar Cissé, kijana kutoka Mali aliyeuawa akiswali ndani ya msikiti.
IQNA – Mshauri wa masuala ya Qur'ani katika Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (A.S) amekutana na Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani ya al-Muzdahar nchini Senegal kujadili njia za kuendeleza ushirikiano.
IQNA – Ayatullah Alireza Arafi, Mkurugenzi wa Vyuo vikuu vya Kiislamu (Hawza) nchini Iran, ametangaza mafanikio makubwa katika elimu ya Qur'ani na taaluma zake, akisisitiza kuanzishwa kwa fani mpya za kielimu, majarida maalumu, na tafsiri mbalimbali ndani ya mtandao wa hawza.
IQNA – Wizara ya Elimu ya Iran inapanga kuanzisha shule rasmi 1,200 mpya za kuhifadhi Qur’ani ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo, kwa mujibu wa afisa mmoja mwandamizi.
IQNA – Mashindano ya 32 ya Kimataifa ya Qur’ani nchini Misri yanatarajiwa kufanyika mwezi Desemba 2025, ambapo toleo la mwaka huu litafanyika kwa kumbukumbu ya Qari maarufu hayati Shahat Muhammad Anwar, mmoja wa wasomaji wenye ushawishi mkubwa wa Qur'ani nchini Misri na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla.
IQNA – Afisa wa afya kutoka Iran amesisitiza umuhimu wa kuzingatia kanuni za usafi na afya wakati wa safari ya Hija ili kuweza kunufaika vilivyo na safari hii ya kiroho.
IQNA – Kituo cha Kitaifa cha Sayansi za Qur'ani, kilicho chini ya Idara ya Waqfu wa Kishia ya Iraq, kinapanga kuandaa kozi za Qur'ani za majira ya kiangazi kwa wanafunzi wa shule.
IQNA-Mwanaume mmoja wa Kifaransa aliyemdunga kisu na kumuua Mwislamu aliyekuwa akisali katika msikiti ulioko kusini mwa Ufaransa, ameshtakiwa rasmi kwa mauaji ya kukusudia yanayochochewa na chuki ya kidini au kikabila, ofisi ya mwendesha mashtaka wa Nîmes ilitangaza Ijumaa.
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ameutaka Ulimwengu wa Kiislamu kutoruhusu suala la Palestina lisahaulike akisisitiza ulazima wa kukabiliana na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.