IQNA

Jumuiya ya Maulamaa wa Kiislamu yafungiwa ukurasa wa Facebook baada ya kutaka Israel isusiwe

18:01 - January 06, 2021
Habari ID: 3473531
TEHRAN (IQNA) – Shirika la mtandao wa kijamii wa Facebook limeufunga ukurasa wa Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Kiislamu (IUMS) baada ya jumuiya hiyo kutoa fatwa yake ya kuwataka Waislamu wasusie bidhaa za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Jumuiya ya Kimataifa ya Maulamaa wa Kiislamu (IUMS), wiki hii ulitoa fatwa ya kuwajibisha kuwekewa vikwazo vya kila upande utawala wa Kizayuni. Fatwa hiyo inasema ni haramu kununua na kuuza bidhaa za utawala wa Kizayuni hadi utawala huo utakapoacha kuzikalia kwa mabavu ardhi za Waislamu.

Jumatano Jumuiya Kimataifa wa Maulamaa wa Kiislamu imetangaza kuwa, uongozi wa Facebook umeufunga ukurasa wake baada ya kutoa fatwa ya kuharamisha kunua na kuuza bidhaa za utawala wa Kizayuni.

Jumuiya hiyo imetoa fatwa hiyo ili kulinda na kuhami uadilifu katika Uislamu hususan kadhia ya Palestina na umesisitiza kuwa utaendelea na msimamo wake huo bila ya kutetereka.

Wito huo unakuja wakati ambao mwaka wa 2020, nchi nne za Kiarabu ambazo ni Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na Morocco zilitangaza kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na hivyo kujiunga na Misri na Jordan ambazo zinautambua utawala huo ghasibu.

Katika miaka ya hivi karibuni mashirika hayo mengi duniani yanaunga mkono vuguvugu la BDS la kuusussia utawala haramu wa Israel kibiashara, kiuchumi, kiutamaduni na kielimu. Vuguvugu hilo la kimataifa la Boycott, Divestment and Sanctions (BDS) linawaunga mkono Wapalestina kwa kuendesha kampeni dhidi ya Israel kwa kuisusia, kuitenga na kutoshirikiana nayo katika uwekezaji.

3946191

Kishikizo: maulamaa BDS israel
captcha