IQNA

Mwezi Mtukufu wa Ramadhan

Siku Kumi za mwisho za Ramadhani zitakuwa likizo nchini Maldives

20:51 - February 06, 2024
Habari ID: 3478313
IQNA - Serikali ya Maldives imetangaza siku kumi za mwisho za mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwa siku za likizo rasmi kwa wafanyakazi wa sekta ya umma.

Rais Mohamed Muizzu alisema ofisi za serikali na taasisi za serikali zitafungwa katika siku kumi za mwisho za Ramadhani, kuanzia siku ya 20 ya mfungo wa mwezi.

Tangazo hilo lilitolewa na Ofisi ya Rais mwishoni mwa juma.

Rais alifikia uamuzi huo kufuatia mijadala iliyowasilishwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu katika kikao cha baraza la mawaziri tarehe 17 Disemba 2023.

Hili limeanyika kwa madhumuni ya kukuza maadili ya Kiislamu ndani ya jamii pamoja na kuhimiza umma kuimarisha ushiriki wao katika masuala ya kidini.

Likizo hiyo inalenga kuwawezesha wananchi kutanguliza ibada katika siku kumi za mwisho za mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Agizo hilo lilibainisha kuwa ofisi za serikali na taasisi za serikali zimeagizwa kuhakikisha huduma muhimu zinatolewa kwa umma, na taarifa mahususi kuhusu saa za kazi katika siku hizi zinatolewa kwa ufanisi.

Ofisi ya Rais ilifanya kikao na mamlaka husika ili kujadili namna ya utoaji wa huduma muhimu katika siku kumi za mwisho za Ramadhani.

3487095

captcha